Soundcloud

Shule 10 Bora matokeo ya Kidato cha Sita 2018 hizi hapa

Leo July 13, 2018 Katibu Mkuu wa Baraza la Mtihani la Tanzania (NECTA) Charles Msonde ametangaza baraza hilo kuzuia matokeo ya watahiniwa 13 kutokana na sababu mbalimbali na wengine 8 kufutiwa kabisa matokeo kwa sababu ya udanganyifu.
 Akizungumza na waandishi wa habari Dkt. Msonde amesema kuna watahiniwa walishindwa kukamilisha mitihani yao kutokana na sababu za kiafya na hivyo kufanya mitihani nusu, watapewa nafasi ya kurudia mwaka unaofuata.
Dkt. Msonde amesema ufaulu umeongezeka kutoka asilimia 96.06% mwaka 2017 hadi97.12% mwaka huu, huku ufaulu katika masomo ya sayansi umeshuka ukilinganishwa na masomo ya sanaa na biashara.
Jumla ya watahiniwa 83,581 sawa na asilimia 97.58 ya waliofanya mitihani ya kidato cha sita May 2018 wamefaulu huku wasichana wakiwa ni 34,358, na wavulana waliofaulu ni 49,223 pekee” 
Dkt. Msonde ameongeza kuwa tathmini ya hali ya matokeo imeonesha kuimarika kwa ufaulu katika madaraja ya I,II na III ikiwemo kupanda kwa asilimia 1.80 kutoka 93.72 mwaka 2017 na kuwa asilimia 95.52 mwaka 2018.
Shule 10 Bora ni Kibaha, Kisimiri, Kemebos na Mzumbe, Feza Boys, Marian Boys, AHMES, St Mary’s Mazinde Juu, Marian Girls & Feza Girls.
CREDIT: MILLARD AYO

Post a Comment

0 Comments