Mtanzania aliyebaki kwenye kikosi cha TP Mazembe Thomas Ulimwengu
alikuwa ni sehemu ya wachezaji waliocheza kwenye mchezo dhidi ya Yanga
na kuisaidia timu yake kupata ushindi wa bao 1-0 na kujiweka pazuri
kwenye Kundi A baada ya kuvuna point sita katika michezo miwili
waliyoshuka dimbani.
Bada ya game kumalizika, ulimwengu amesema siri ya ushindi ya Mazembe
inatokana na muunganiko wa professional players wengi wenye uzoefu
kwenye timu yao.
“Nilisema mwanzoni kwamba tunakuja kuchukua ushindi, Yanga ni timu nzuri
kama mlivyoona wamecheza vizuri lakini kama professional players wengi
wenye uzoefu tumeonesha uwezo wa kupata ushindi kwenye mechi ya leo”,
amesema Ulimwengu ambaye awali alisema yeye amekuja kucheza nyumani na
siyo ugenini.
“Nawapa changamoto wachezaji wa Tanzania watoke wengi tupate professionals wengi ili tuweze kuisaidia timu yetu ya taifa.”
“Yanga bado wananafasi, mechi bado ni nyingi wakishinda wanaweza
wakapita kwenye kundi na kwenda hatua inayofuata”, alimaza nyota huyo wa
Stars ambaye kocha wake pia alimwagia sifa lukuki kutokana na kiwango
alichokionesha kwenye mchezo wa leo.





0 Comments