Soundcloud

Video: Kanye West awachana Jay Z, Beyonce na vituo vya redio, akatisha show katikati

Kanye West alikatisha show iliyokuwa imehudhuriwa na mashabiki zaidi
ya 13,000 huko Sacramento, Calif., Jumamosi hii baada ya kuwashushia
mabomu Beyonce na Jay Z.



“Get ready to have a field day, press, because the show’s over,” staa
huyo alisema baada kuitupa mic kwenye ukumbi wa Golden 1 Center.


Mashabiki waliokuwa wamelipa zaidi ya $250 kwenye ziara yake ya
‘Saint Pablo Tour’ walichukizwa na kuanza kutaja jina la rapper huyo
kumlaani kwa kukatisha show yake.


Mashabiki hao walidaiwa kusubiri kwa zaidi ya saa moja ili apande
jukwaani. Na baada ya kutumbuiza nyimbo 3 kwa kurudia wimbo mmoja huku
akitumia zaidi ya dakika 10 kuzungumza masuala kibao.


Katika malalamiko yake, Yeezy alisema aliumizwa baada ya kumsikia
Beyonce akidai asingetumbuiza kwenye tuzo za MTV kama asingeshinda video
ya mwaka kwa wimbo wake Formation dhidi ya video yake Famous na Hotline
Bling ya Drake.


“Beyonce I was hurt because I heard you said you wouldn’t perform
unless you won video of the year over me and over Hotline Bling. In my
opinion – now don’t go dissing Beyoncé, she’s great. Taylor Swift is
great. We are all great people. But sometimes we be playing the politics
too much and forget who we are – just to win,” alisema Kanye.


Pia alimtaka Jay Z kwa mara nyingine ampigie simu kama mwanaume.


“I know you got killers. Please don’t sent them at my head,” alisema.
Alivishua madongo pia vituo vya redio akidai kuwa vimekuwa na upendeleo
kwa baadhi ya wasanii.


Post a Comment

0 Comments