Mara tu baada ya EMA kueleza kinagaubaga jinsi walivyokosea kumpa Tuzo
Wizkid badala ya Alikiba ,vyombo vya habari vya burudani nchini Nigeria
vimemwelezea Alikiba kama msanii aliyepaswa kubeba tuzo ambayo Wizkid
amechukua.
Kitu kilichoibua hoja zaidi ni baadhi ya mashabiki wa East Africa kuja
juu na kudai kuwa msanii wao yuko vizuri kuliko Wizkid kitu ambacho
kiliandikwa pia na vyombo vya habari huko ikiwemo magazeti, blog na
redio...
Baadhi ya watu walionekana kushangaa lakini huku wengine walidai ni msanii aliyeko chini ya Sony.
Post ya Alikiba iliyoeleza uungwana wake kuhusu wanao mtukana Wizkid
imeandikwa pia katika vyombo vya habari pia TV mbalimbali zimetoa habari
hii.
Hapo karibuni kuna mitandao iliyoeleza uwepo wa msuguano baina ya Wizkid
na Alikiba juu ya nani atangulie stejini na chombo hicho kimeeza kuwa
hiyo ilipelekea kuchelewesha show lakini haikuwa proved kama ndivyo...




