Clouds
TV ipo kwenye kitimoto baada ya kipindi chake cha Take One
kinachoendeshwa na Zamaradi Mketema kumhoji shoga maarufu jijini Dar es
Salaam.
Pamoja na Zamaradi kudai kuwa na nia njema ya kumhoji mtu huyo kwa madai
suala hilo limekuwa tatizo nchini na ni muda wa kulizungumzia bila
kificho, Watanzania wengi wameonesha kupinga kwa madai kuwa kipindi
hicho kimetumika kulitangaza zaidi tatizo hilo.
Wapo pia wanaomtetea Zamaradi na hivyo kusababisha kuwepo na mgawanyiko
mkubwa wa kimsimamo kuhusiana na suala hilo kama Tanzania imefikia hatua
ya kuwepo mijadala ya aina hiyo kwenye runinga za taifa, seuze kuwahoji
kabisa watu hao.
Hata hivyo Jumatano hii Clouds TV imelazimika kufanya kile
kinachojulikana kama ‘damage control’ kujaribu kufafanua kwa wananchi
kwanini ilikuwa sawa kuwa na kipindi cha aina hiyo.
“Suala hili ukilitazama positively utapata kujifunza mengi sana, hiki ni
kipindi cha toba na kuhamasishana mema na kuacha mabaya, hili ni baya
na lazima tulipinge na kulikemea na tusiwaangalie mashoga pekee
tuwaangalie pia wale wanaoshirikiana nao ambao tuko nao ndani ya jamii,”
alisema Zamaradi kwenye kipindi cha 360 cha kituo hicho alipohojiwa
kueleza kwanini aliamua kufanya mahojiano na mtu huyo.
“Tusisubiri mambo yaharibike zaidi ndio tuanze kuzungumza lazima
tuchukuwe hatua sasa, kama tunavyoweza kumhoji mwathirika wa madawa ya
kulevya na kuamini kwa kujua njia alizopitia tutaweza kuepuka na
kuwaelimisha ndugu na jamaa zetu ndivyo hivyo tujifunze walipokosea
hawa,” alisisitiza.
“Je kuna tamthilia ngapi za nje zinaonekana kwenye runinga zetu zenye
maudhui yenye hulka kama hizi na utofauti wa kipindi nilichofanya na
tamthilia za nje ni kwamba kipindi changu kimelenga kukemea na
kufundisha,kikubwa shtuka na chukua hatua. Leo ukienda kwenye kumbi za
starehe kwenye taarabu haya yamekuwa ni mambo ya kawaida na pia ukipita
Instagram utakuta page zao kabisa.”
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alipiga simu kwenye 360 na kutetea kurushwa kwa kipindi hicho.
“Hatuwezi kubadilika kwa kuendelea kuishi katika mazingira tuliyoyazoea,
tunakaa kwenye mazingira kama vile tupo sawa na akija wa kutuambia
hatupo sawa tunawakebehi na kuwashambulia,” alisema Makonda.
“Tuamke na hizi hasira tuelekeze kwenye tatizo ambalo lipo kwenye jamii
yetu, wazazi na walezi tujenge tabia ya kukagua watoto wetu tukiamka pia
majirani zetu. Sisi kama Serikali tumeamshwa na pia inabidi waanze
kutaja wateja wao ili jamii iwafahamu kwani inawezekana wateja wao
wengine ni viongozi wa serikali,” aliongeza.
Hata hivyo bado wananchi wengi wameendelea kusisitiza kuwa kipindi hicho
kimekiuka misingi ya utangazaji na kuitaka TCRA ichukue hatua.
Hizi ni baadhi ya barua zilizotukwa kwenye mamlaka hiyo ya mawasiliano kulalamikia kipindi hicho.
Bonyeza HAPA
kudownload application ya UDAKU SPECIAL kwenye simu yako








0 Comments