Soundcloud

Mchungaji awaomba waumini wamchangie tsh bil. 123 anunue ndege binafsi, amtolea mfano Yesu

Muhubiri maarufu nchini Marekani anayejulikana kama Jesse Duplantis amewataka waumini wake wamnunulie ndege mpya aina ya Dassault Falcon 7X yenye thamani ya dola za kimarekani Milioni 54 sawa na zaidi ya Bilioni 123 za kitanzania.
Muhubiri huyo anasema kuwa Mungu ndio alimwambia aamini katika ndege hiyo ya Falcon 7X na alipomuuliza Mungu atawezaje kupata fedha ya kununua ndege hiyo, Mungu alimjibu kuwa hatakiwi yeye kuinunua ndege hiyo bali anachotakiwa ni kuamini tu katika ndege hiyo.
Hivyo amewaomba waumini wake kujiunga kusali kwa ajili ya kuwa washirika wa kuipata ndege hiyo kwani itaenda kugusa maisha ya watu na kuyabadilisha duniani kote.
Pia muinjilisti huyo aliongeza kwa kusema kuwa kama Yesu Kristo angekuwepo duniani leo basi angetumia usafiri wa ndege kuzunguka dunia nzima.
Kwa sasa muhubiri huyo anamiliki ndege binafsi tatu ambazo zote waumini wake ndio wamemnunulia na macho yake kwa sasa yapo kwenye ndege aina Falcon 7X anayodai itamwezesha kusambaza huduma ya Mungu duniani kote.

Post a Comment

0 Comments