Kumekuwa na sintofaham kwa mashabiki wa kundi la vichekesho la original
comedy la hapa nchini linaloundwa na vijana sita akiwemo Mpoki, Masanja,
Joti, Mark Regan kipara na wengineo kwa kuwataja wachache kwamba huenda
hilo kundi limevunjika na pengine kuna beef kati ya kutokana na
mfululizo wa matukio ya hivi karibu.
1. Kutokutoa kazi mpya kwa muda mrefu
Kubwa ni ukimya wa hili kundi wa kutoa kazi mpya. Wamekuwa kimya sana
hawa wasanii kwenye kutoa kazi mpya kupelekea watu kujiuliza pengine
limekufa.
2. Kila mtu anafanya kazi yake
Kwa sasa kila mtu anafanya kazi yake kwa Mpoki yeye ni muajiriwa kituo
cha radio cha E fm. Masanja amejiajiri kwenye miradi kadhaa ikiwemo ule
aliofungua muda si mrefu wa uuzaji mgahawa.
3. Kutokushirikiana kwenye shughuli za kijamii
Kwa sasa baadhi ya hawa wasanii wamekuwa hawahudhurii kwenye baadhi ya
shughuli za kijamii ikiwemo harusi na sherehe. Mfano hivi karibu mmoja
kati ya hawa wasanii Masanja alikuwa anaoa. Wengi walihudhuria lakini
Mpoki hakuonekana kwenye shamrashamra za harusi hiyo kuweza kutia hofu
kwa mashabiki zao.
Je kundi limekufa?




